Ushiriki wa Atabatu Abbasiyya tukufu katika kongamano la kimataifa kuhusu mchango wa maktaba katika maendeleo endelevu

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu imepiga hatua kubwa katika kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu, kwenye nyanja tofauti, hatua hizo imekua sababu kubwa ya watu mbalimbali kutoka ndani na nje ya Iraq kutembelea maktaba yetu na kuangalia mafanikio hayo, hivyo kituo cha faharasi na kupangilia taaluma chini ya maktba na Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya kimeshiriki kwenye makongamano na nadwa nyingi, ikiwa ni pamoja na ushiriki huu kwa njia ya mtandao unaofanyika kwa mara ya kwanza chini ya uratibu wa kitivo cha sayansi wa binaadamu na jamii/ kitengo cha elimu ya Habari na mawasiliano na elimu ya maktaba katika taifa la Aljeria.

Kongamano hili linahusu mchango wa maktaba na taasisi za elimu katika kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu, mkuu wa maktaba Ustadh Hasanaini Mussawi kwa kushirikiana na Dokta Azhari Zairu Jaasim kutoka chuo kikuu cha Mustanswariyya wamewasilisha mada iliyokua na anuani isemayo: (Nafasi ya kituo cha faharasi na kupangilia taaluma katika kutoa sauti ya maktaba za Iraq kwenye mtandao wa ramani ya maktaba -IFLA Library Maps of the World-). Mada hiyo imejikita katika kuonyesha mifano na uzowefu wa maktaba na taasisi za elimu katika kufanyia kazi maendeleo endelevu kwenye jamii.

Imepata muitikio mkubwa, kulikua na michango tofauti pamoja na maswali ambapo wawasilishaji wa mada walijibu na kufafanua zaidi pale palipohitaji ufafanuzi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: