Toleo la kitabu cha kumi na moja katika mfululizo wa Qur’ani katika masomo ya kimagharibi

Maoni katika picha
Kituo cha kiislamu na masomo ya kimkakati chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimetoa juzu la pili la kitabu cha (Qur’ani na mustashriquna.. tafiti za mustashriquna kuhusu Qur’ani tukufu), nalo ni toleo la kumi na moja katika mfululizo wa Qur’ani katika tafiti za kimagharibi.

Mkuu wa kituo hicho Sayyid Hashim Milani ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kitabu hiki ni muondelezo wa kitabu kilicho tangulia juzu la kwanza, maudhui zake zimegawanywa sehemu tatu, kila sehemu imejaa mada za kitafifi, zimeandikwa na watafiti waliobobea katika fani hiyo”.

Akaongeza kuwa: “Kila sehemu inamlango unaofafanua mtazamo wa kiislamu kwa ujumla kuhusu mambo yaliyo andikwa kwenye sehemu hiyo, kama ifuatavyo:

Sehemu ya kwanza: Mustashriquna na tafsiri ya Qur’ani.

Sehemu ya pili: Mustashriquna Mayahudu na Qur’ani tukufu.

Sehemu ya tatu: Utafiti katika mada za Qur’ani zilizotolewa na baadhi ya Mustashriquna.

Tambua kuwa kitabu hiki ni sehemu ya mfululizo wa vitabu vya Qur’ani katika tafiti za kimagharibi, vinavyo andikwa na kituo kwa lengo la kuondoa utata na upotoshaji, uliozushwa au kuwekwa na Mustashriquna na wengineo wanaotaka kupotosha Qur’ani tukufu, hakika Qur’ani itaendelea kuwa kitabu kitakatifu cha Mwenyezi Mungu kinacho ongoa walimwengu na sheria bora katika Maisha ya duniani.

Kuangalia lakala laini ya kitabu kwa njia ya mtandao fungua link ifuatayo: //www.iicss.iq/?id=3409

Pia unaweza kutembelea maonyesho ya vitabu katika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu, au maonyesho ya Atabatu Abbasiyya ya vitabu katika barabara ya Rasuul Najafu Ashrafu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: