Vikao vya kujadili mkakati wa malezi na ufundishaji vinaendelea

Maoni katika picha
Kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu kinaendelea na vikao vya watumishi wa idara na kamati tendaji za shule za Al-Ameed, kujadili mkakati wa malezi na ufundishaji unaotarajiwa kutekelezwa katika mwaka mpya wa masomo.

Rais wa kitengo Dokta Ahmadi Swabihi Ka’abi amesema: “Kitengo kiliandaa mkakati wa (mwaka wa masomo 2021 – 2022), wenye vipengele vingi vinavyo lenga kuboresha sekta ya malezi na elimu, kwa kutumia mbinu za kisasa, kufuatia kuingia mwaka mpya wa masomo watumishi wamekua na vikao vya kujadili utekelezaji wa mkakati huo”.

Akaongeza kuwa: “Kwa ajili ya kuboresha utendaji na utekelezaji wa mkakati huo, tumekua tukijadili na kufafanua vipengele muhimu kiofisi na kiutendaji, ili kuhakikisha unatekelezwa kama ulivyo pangwa”.

Akamaliza kwa kusema: “Mikutano hii ni kwa ajili ya kukazia maarifa na kuhakikisha tunafanya kazi kwa timu, na kulinda uzowefu uliopo katika shule za Al-Ameed”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: