Makumi ya vijana wanakuja Atabatu Abbasiyya kufunga ndoa na wenza wao

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia kitengo cha Dini, imeshuhudia vijana wengi wakija kufunga ndoa, kwa ajili ya kutabaruku na mwenye malalo hii takatifu Abulfadhil Abbasi (a.s) na kufuatia matukio matukufu yaliyopo ndani ya mwezi wa Rabiul-Awwal, ambapo tukio la kwanza lilikua ni kuvishwa taji la uongozi Imamu Mahadi (a.f), na mwisho tukio la kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) sambamba na kumbukumbu ya kuzaliwa mjukuu wake Imamu Swadiq (a.s).

Makamo rais wa kitengo tajwa Shekh Aadil Wakili ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Tumefanikiwa kufungisha ndoa katika mwezi wa Muharam na Safar, na ulipoingia mwezi wa Rabiul-Awwal tumeendelea kufungisha ndoa nyingi kupitia idara ya ndoa za kisheria, kuna ongezeko kubwa la idadi ya ndoa zinazo fungishwa, jambo hili limezoweleka kila mwaka, siku kama hizi huwa kunakua na ongezeko kubwa la watu wanaofunga ndoa kutoka ndani na nje ya Karbala”

Akaongeza kuwa: “Ndoa zinafungishwa kwa kufuata utaratibu maalum, ikiwa ni pamoja na uwepo wa wasimamizi wa mwanaume na mwanamke, na kutangaza kukubali mume kwa pande zote mbili, ndoa inaongozwa na mmoja wa Masayyid au Mashekhe wanaotoa huduma katika kitengo cha Dini, sambamba na kuwaombea dua ya kuwa na maisha mema ya ndoa, kisha wanandoa kupewa nasaha na kufafanuliwa umuhimu wa maisha ya ndoa na ahaki za mume na mke na wajibu wao, kupitia riwaya za maimamu watakatifu (a.s) na hadithi tukufu”.

Kumbuka kuwa miongoni mwa harakati za kitengo cha Dini ni kufungisha ndoa bure, kuna ratiba maalum ya kufungisha ndoa kwa kuzingatia baadhi ya siku ambazo ni makuruhu kufunga ndoa katika mwana, sambamba na siku za kumbukumbu za vifo vya maimamu watakatifu (a.s) na mwezi wa Muharam na Safar.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: