Kituo cha ufundishaji wa sekta ya habari kinatoa mafunzo ya upigaji wa picha kwa watumishi wa makumbusho ya Alkafeel

Maoni katika picha
Kituo cha ufundishaji wa sekta ya habari chini ya kitengo cha habari katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kinatoa mafunzo ya upigaji wa picha kwa watumishi wa kitengo cha makumbusho ya Alkafeel, kwa lengo la kuongeza kiwango chao cha ujuzi katika sekta hiyo, na kuwaonyesha program za kisasa katika fani hiyo muhimu kwa maeneo mengi ya makumbusho.

Semina imefanywa ndani ya ukumbi wa Qassim (a.s) chini ya ukufunzi wa kiongozi wa idara ya upigaji wa picha katika idara ya uzalishaji wa vipindi Alkafeel Sayyid Saamir Husseini, amefundisha mada nyingi zinazo hitajiwa na kundi hilo katika shughuli zao.

Husseini ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Mada zote za msingi anazotakiwa kufahamu mpiga picha zimefundishwa, kama vile misingi ya picha za rangi, aina za kamera, maneno maarufu katika fani ya upigaji wa picha, kwa mfano kupangilia mwanga, kupanga rangi, vifaa vinavyo hitajika katika upigaji wa picha, tofauti za mionzi ya kamera, matumizi ya flashi wakati wa kupiga picha, namna ya kuandaa studio ya picha, na upigaji wa picha za haraka”.

Akaongeza kuwa: “Hali kadhalika wameambiwa baadhi ya changamoto kubwa ambazo hutokea kwa mpiga picha, kwa mfano: mwanga kwenye sehemu za wazi, tatizo la mstari mweusi unaoweza kutokea kwenye picha inayopigwa studio, umuhimu wa kupiga picha kwa kusimama sehemu muwafaka, mwanga unaotosha na wenye muonekano mzuri”.

Kumbuka kuwa kituo cha kufundisha masomo ya habari, ni miongoni mwa vituo muhimu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimesha ratibu semina nyingi za mambo ya habari chini ya wakufunzi wenye uzowefu mkubwa sambamba na kutumia wakufunzi kutoka nje ya Ataba tukufu, mafunzo hayo yamekua na matokea mazuri katika kazi zao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: