Kuratibu mashindano ya Qur’ani kwa mara ya kwanza yanayo husisha wasio ona

Maoni katika picha
Kitengo cha masomo ya Qur’ani chini ya chuo kikuu cha Ummul-Banina (a.s) cha wasichana katika Atabatu Abbasiyya, kimeendesha shindano la Qur’ani kwa wanawake la kuhifadhi Qur’ani kwa kuzingatia mada za Qur’ani linalo husisha watu wenye ulemavu wa macho (wasio ona), nalo ni shindano la kwanza hapa Iraq.

Rais wa kitengo hicho Ustadh Ali Bayati ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Shindano limeandaliwa na kuratibiwa kwa ufadhili wa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu, nalo ni miongoni mwa mashindano yanayo simamiwa na kitengo cha masomo ya Qur’ani, shindano hili ni la aina yake na marachache kufanyika hapa Iraq, aidha lina umuhimu mbukwa katika jamii ya waislamu, hususan wale ambao ni vigumu kwao kuhifadhi Qur’ani yote kwa sababu moja au nyingine”.

Akaongeza kuwa: “Shindano lemeandaliwa katika mazingira yanayo endana na wahusika, chini ya kamati ya majaji waliobobea, washiriki ni wasichana wasio ona kutoka mikoa tofauti ya Iraq, limefanywa kupitia jukwaa la (Google meet), taasisi ya wasomi wa Qur’ani wasio ona imeshiriki, kulikua na kamati ya majaji waliobobea katika sekta ya kuhifadhi Qur’ani kwa maudhui”.

Akabainisha kuwa: “Shindano limekamilika kwa kupata washindi wafuatao:

Mshindi wa kwanza: Ruqayya Adiib/ Bagdad.

Mshindi wa pili: Aayah Imaad/ Diyala.

Mshindi wa tatu: Aayaatu Dhiyaau/ Bagdad.

Mshindi wa nne: Fatuma Muhammad/ Basra.

Mshindi wa tano: Hanani Muftan/ Basra”.

Kumbuka kuwa hili ni shindano la pili kufanywa na kitengo cha masomo ya Qur’ani katika upande wa kuhifadhi kwa maudhui ya Qur’ani tukufu, kwa lengo la kuelewa maudhui za Qur’ani kama aqida, hukumu, sheria, tabia na nyinginezo, kwa kuwataka washiriki wahifadhi aya zinazo fundisha mambo mbalimbali ndani ya Qur’ani pamoja na kuzisherehesha kwa ufupi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: