Kuweka mfumo wa kamera za ulinzi za kisasa zaidi katika malalo ya Atabatu Abbasiyya tukufu

Maoni katika picha
Idara ya mawasiliano na teknolojia chini ya kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imekamilisha kuweka mfumo wa kamera za ulinzi za kisasa na zenye ubora mkubwa hapa Iraq.

Kiongozi wa idara Mhandisi Farasi Abbasi Hamza, ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Tangu tulipoweka mfumo wa kamera za ulinzi mwaka (2016) zilizokua ni toleo la pili la aina hiyo, tumekua tunafanyia kazi maelekezo ya uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu, ya kujitahidi kwenda na maendeleo katika vitu vinavyoshuhudia maendeleo ya kazi, tumeweza kwenda sambamba na maendeleo kama yanavyojitokeza hadi leo tumefika hapa, kamera hizi ni toleo la tatu katika teknolojia hii”.

Akaongeza kuwa: “Kazi ya uboreshaji na ufungaji wa vifaa iligawanyika sehemu mbili:

Sehemu ya kwanza: Kubadilisha kamera zote za toleo la pili na kuweka za toleo la tatu, tambua kuwa idadi yake ilikua mamia.

Sehemu ya pili: Kujenga sehemu za kufunga kamera zaidi ya (1300) kutoka kamera (600) zilizokuwepo awali, pamoja na kubadilisha mfumo wa uwekaji wa kamera kutokana na teknolojia ya kamera za sasa”.

Akabainisha kuwa: “Kamera mpya zinaubora mkubwa na zinaonyesha eneo kubwa zaidi, zinauwezo wa kuonyesha picha nzuri kwenye giza nene, pia zinauwezo wa kukuza picha mara nne zaidi ya kamera za zamani, kamera hizi ndio toleo jipya linalotegemewa duniani kwa sasa”.

Akaongeza: “Mfumo mpya wa kamera unauwezo mkubwa wa kupiga picha za video na kuzituma kwenye vitengo tofauti vya Ataba tukufu, kwa lengo la kutoa huduma kwa mazuwaru watukufu au kuboresha huduma zinazo tolewa, pamoja na kuimarisha ulinzi na usalama na kudhibiti wahalifu wanaotaka kuharibu sifa ya eneo hili takatifu, tambua kuwa mfumo huu umetengenezwa kwa teknolojia ya kizazi cha nne inayotumia utambuzi kwa njia ya teknolojia”.

Akafafanua kuwa: “Kamera zimefungwa kulingana na mahitaji, zimewekwa sehemu zote za Atabatu Abbasiyya tukufu, kuanzia ndani ya haram tukufu, kwenye ukumbi wa haram na eneo lote la nje linalo zunguka haram, na kwenye barabara zilizo karibu na haram, na kwenye majengo ya nje, tunaweza kuongeza kamera zingine wakati wowote na mahala popote tutakapoona kunahaja ya kuweka kamera”.

Akamaliza kwa kusema: “Kazi ilikamilika ndani ya muda uliopangwa chini ya idara mbili bila kutegemea msaada kutoka nje, kazi hii zamani ilikua inaigharimu Atabatu Abbasiyya hela nyingi, tuliifanyia majaribio katika ziara ya Arubaini na ikaonyesha mafanikio makubwa, na sasa hivi inafanya vivuri tunamshukuru Mwenyezi Mungu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: