Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu amehudhuria uwekaji wa jiwe la msingi kwenye jingo la polisi wa kulinda haram mbili tukufu

Maoni katika picha
Ugeni kutoka Atabatu Abbasiyya tukufu ukiongozwa na katibu mkuu Mhandisi Muhammad Ashiqar leo siku ya Jumapili (1 Rabiul-Aakhar 1443h) sawa na tarehe (7 Novemba 2021m) umeshiriki kwenye hafla ya kuweka jiwe la msingi kwenye jengo la polisi wa kulinda malalo mawili matakatifu, mbele ya mkuu wa mkoa wa Karbala Mhandisi Naswifu Jaasim Khatwabi na kamanda wa polisi.

Mkuu wa mkoa wa Karbala amesema: “Katika kukamilisha safari ya ujenzi unaofanywa na serikali ya mkoa kila mahala, sawa iwe kwenye taasisi za kutoa huduma kwa jamii, ulinzi au elimu, watumishi wamekua wakifanya kazi kubwa ya kuendeleza ujenzi huo”.

Akafafanua kuwa: “Polisi wa mkoa wa Karbala wanafanya kazi kubwa wakiwa na ari ya hali ya juu, ya kuhudumia wageni wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), katika kuwatendea haki na kuendelea kuwatia moyo tumeamua kujenga jengo maalum la polisi wanaolinda haram mbili takatifu”.

Kumbuka kuwa polisi wa haram mbili tukufu ni sehemu ya vikosi vya jeshi, wanafanya kazi bega kwa bega na kitengo cha kulinda nidham cha Atabatu Husseiniyya na Abbasiyya, wamekua wanashirikiana kuimarisha ulinzi kwa mazuwaru katika kila kitu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: