Shirika la Khairul-Juud limehitimisha ushiriki wake katika maonyesho ya kwanza ya kilimo

Maoni katika picha
Shirika la teknolojia ya kilimo cha kisasa Khairul-Juud chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, limekamilisha ushiriki wake kwenye maonyesho ya bidhaa za kilimo yaliyofanyika Arbiil mara ya kwanza kwa muda wa siku tatu, ushiriki huu ulikuwa na mafanikio sawa na awamu zilizo tangulia za ushiriki wa maonyesho ya kitaifa na kimataifa, shirika limefanikiwa kutuma ujumbe wa kuonyesha hali halisi ya kilimo hapa nchini, kupitia bidhaa zake za mbolea na pembejeo zingine zinazo tengenezwa hapa Iraq kwa ubora mkubwa.

Tawi la shirika letu lilikua kituo muhimu kwenye maonyesho haya, na limepata mwitikio mkubwa, jambo ambalo limepelekea uongozi wa tawi kupewa zawadi na shirika kuu la kilimo chini ya wizara ya kilimo ya Iraq, kama sehemu ya kupongeza kazi nzuri inayofanywa.

Kumbuka kuwa kushiriki kwenye maonyesho ni fursa kubwa ya kuonyesha maendeleo ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kwenye sekta ya kilimo, ujenzi na ufugaji, sambamba na kuongeza uwezo wa upatikanaji wa chakula kitaifa, hali kadhalika ni sehemu ya kuonyesha maendeleo ya teknolojia inayotumika kwenye sekta ya kilimo kwa sasa, pamoja na kubadilishana ujuzi na uzowefu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: