Kituo cha turathi za Basra na nafasi yake katika kuhuisha turathi

Maoni katika picha
Kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kinavituo kadhaa vya turathi, vyenye jukumu la kuhuisha na kulinda turathi za maoneo yao, miongoni mwa vituo vinavyo husika na kuhuisha turathi za Dini, adabu, historia na fani za watu ni kituo cha turathi za Basra.

Kituo kinaongozwa na watu wenye uwezo mkubwa, ambao ni wasomi wa hauza na sekula, kinatumia mbinu tofauti kufikia malengo, miongoni mwa mbinu hizo ni:

  • - Kufanya uhakiki, kuandika na kutangaza.
  • - Kufanya nadwa na makongamano.
  • - Kuendesha semina, kituo kimefanikiwa kutoa machapisho mbalimbali (158) ndani ya miaka sita.
  • - Kufungua mlango wa kushirikiana kielimu na kimaarifa na taasisi za kitamaduni na kielimu katika mji wa Basra, kituo hupokea wadau na wasomi wa turathi karibu kila siku.

Kituo ni ofisi muhimu sana, inawapigapicha wa malikale za Basra na zisizokua za Basra (278), na waandishi wa sayansi ya binaadamu, historia, maarifa ya Qur’ani, tafsiri, na mengineyo kama vile, vitabu, faharasi, maandiko ya tafiti za digrii ya pili na ya tatu.

Kumbuka kuwa kituo kimeandika vitabu vingi vyenye maudhui tofauti, bado kuna ambavyo vipo katika hatua ya uandishi, na vinatarajiwa kukamilika hivi karibuni, bila shaka vitaongeza kitu katika maktaba za kiislamu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: