Kuanza semina ya kuandaa mpango kazi katika program ya kujenga uwezo kwenye mambo ya kiutawala

Maoni katika picha
Kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu kimeanza semina iitwayo (Uandaaji wa mpango kazi) inayo husisha marais wa vitengo na wasaidizi wao katika Atabatu Abbasiyya tukufu.

Rais wa kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu katika Atabatu Abbasiyya tukufu Dokta Muhammad Hassan Jaabir amesema: “Semina hii ni sehemu ya kukamilisha program ya kujenga uwezo katika mambo ya kiutawala, inamada nyingi, miongoni mwake ni: Mpango kazi, dira, utume, misingi, malengo pamoja na App ya SWOT na PESTEL na mambo mengine yanayo fungamana nayo, kuweka utekelezaji wa mambo hayo”.

Akaongeza: “Semina itafanyika kwa muda wa siku tano na itakuwa na mada zifuatazo:

  • - Mbinu kuu za kuandaa mpango kazi, ufuatiliaji, tathmini na usimamiaji wa kazi.
  • - Uwezo wa kufikiri kiubunifu.
  • - Kufanya upembuzi yakinifu.
  • - Kutambua mifano muhimu katika misingi ya kiidara.
  • - Kufanya maendeleo na mabadiliko.
  • - Kupata mbinu za utendaji kiidara.
  • - Utekelezaji wa miradi”.

Tambua kuwa semina hii ni sehemu ya mradi mkubwa wa mafunzo ya kiidara, unayotolewa kwa viongozi wote wa Atabatu Abbasiyya tukufu, kwa lengo la kujenga uwezo wa kiutendaji kwa kutumia mbinu za kisasa, jambo ambalo husaidia ushirikiano kati ya viongozi na wasio viongozi, na kuhakikisha zaairu wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) anapata huduma bora.

Kumbuka kuwa program hii inatokana na ushauri wa uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya, chini ya Mheshimiwa kiongozi mkuu wa kisheria Sayyid Ahmadi Swafi na katibu wake mkuu, kwa lengo la kuifanya Atabatu Abbasiyya kuwa taasisi inayofuata taratibu bora katika nyanja zote.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: