Kusaini nyaraka za ushirikiano wa kielimu baina ya chuo kikuu cha Alkafeel na Dhiqaar

Maoni katika picha
Rais wa chuo cha Dhiqaar Dokta Yahya Abduridhwa Abbasi akiwa na viongozi wa vitivo na marais wa vitengo, asubuhi ya Jumanne wametembelea chuo kikuu cha Alkafeel kilicho chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, wamekagua madarasa na vyumba vya maabara, wakiwa pamoja na rais wa chuo kikuu cha Alkafeel Dokta Nuris Dahani.

Mwisho wa matembezi yao wamesaini mkataba wa ushirikiano wa kielimu kati yao, na kubadilishana uzowefu wa kielimu katika mambo tofauti.

Dokta Yahya Abduridhwa Abbasi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Leo tumekuja kutembelea kituo hiki muhimu cha elimu, tumeangalia madarasa, maabara, na vifaa vya kusomea kwa njia ya uhudhuriaji na mtandao, ambavyo vimechangia kuboresha mazingira ya chuo na kukifanya kuwa bora kwa wanafunzi wa Iraq”.

Akasisitiza kuwa: “Chuo hiki ni fahari kwa wairaq, tumeona utaratibu mzuri wa kisasa walio nao, pamoja na walimu mahiri wenye weledi mkubwa, jambo ambalo matunda yake yanaonekana wazi kwa wanafunzi wao”.

Akafafanua kuwa: “Tumesaini makubaliano ya ushirikiano wa kielimu, chini ya muongozo wa wizara ya elimu na tafiti za kielimu, makubaliano haya yanafungua milango ya ushirikiano baina ya vyuo hivi viwili, sambamba na kufanya semina, warsha na miradi ya kitafiti kwa ushirikiano, aidha itaundwa kamati ya kufanya tafiti itakayo jumuisha wajumbe kutoka vyuo vyote viwili, tunaamini makubaliano yatatekelezwa kama yalivyo pangwa”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: