Kitengo cha malezi na elimu ya juu kinafanya semina ya kuwajengea uwezo walimu wa shule ya awali katika mkoa wa Dhiqaar

Maoni katika picha
Kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kinafanya semina kwa walimu wa shule za awali na vituo vya kulea mayatima katika mkoa wa Dhiqaar.

Mkufunzi wa semina Ustadh Falahu Juma amesema: “Semina inahusu (mbinu za kubadilisha tabia), kutambua tabia na aina zake, na vigezo vinavyotumika kubaini tabia za mtoto, sambamba na kuwafundisha walimu mbinu za ulezi wanazo weza kutumia katika kuamiliana na aina tofauti za watoto”.

Akaongeza kuwa: “Lengo la msingi katika semina hiyo ni kuwafundisha walimu njia za kuwafanya watoto kuwa na tabia nzuri, na kuwazuwia wasiwe na tabia mbaya, na kuwafanya watii misingi ya Dini tukufu ya kiislamu”.

Tambua kuwa semina hii ni sehemu ya ushirikiano kati ya Atabatu Abbasiyya na taasisi za malezi na elimu, kwa lengo la kuwajengea uwezo walimu kupitia semina mbalimbali.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: