Shirika la Khairul-Juud limekamilisha maandalizi ya kwenda kushiriki maonyesho ya biashara yatakayofanyika Basra

Maoni katika picha
Shirika la Khairul-Juud limekamilisha maandalizi ya kushiriki kwenye maonyesho ya biashara ya kimataifa yatakayo fanyika kuanzia tarehe (10 – 20 Novemba).

Mkuu wa shirika Ustadh Maitham Bahadeli amesema: “Shirika la Khairul-Juud katika ushiriki huo, linatarajia kufungua mlango wa mawasiliano na mashirika ya kitaifa na kimataifa, na kuangalia maendeleo ya kisasa katika sekta ya utengenezaji wa mbolea na kilimo, pamoja na mambo mengine yanayo tengenezwa na shirika la Khairul-Juud”.

Akaongeza kuwa: “Lengo lingine la kushiriki kwenye maonyesho hayo ni kutambulisha bidhaa zinazo tengenezwa na shirika letu kwenye mashirika mengine, na maendeleo tuliyo fikia, baada ya kuboresha uzalishaji”.

Akaendelea kusema: “Kuna mashirika mengi makubwa yanashiriki kwenye maonyesho ya biashara ya Basra, moanyesho hayo yanatembelewa na watu kutoka mikoa yote ya Iraq na mashirika mbalimbali, hivyo kushiriki kwenye maonyesho hayo ni fursa nzuri ya kutambulisha bidhaa zetu”.

Kumbuka kuwa shirika la Khairul-Juud, hivi karibuni lilishiriki kwenye maonyesho ya kilimo na mazao ya wanyama yaliyofanyika Arbiil, ushiriki ulikua wenye mafanikio makubwa, shirika lilitunukiwa tuzo na uongozi wa maonyesho hayo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: