Idara ya Tahfeedh inaendelea kufanya mashindano ya kila mwezi kwa wanafunzi wake wa Karbala

Maoni katika picha
Idara ya Tahfeedh chini ya Maahadi ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya tukufu, inaendelea na mashindano ya kila mwisho wa mwezi kwa wanafunzi wake, ili kuimarisha uwezo wao.

Mashindano hayo hufanywa ndani ya ukumbi wa jengo la Alqami katika Atabatu Abbasiyya tukufu, wanafunzi waliohifadhi Qur’ani ndio washiriki wa mashindano hayo, kamati ya majaji huwauliza maswali tofauti, kama namba za kurasa, namba za aya, aya ya kwanza kwenye ukurasa, aya ya mwisho, na mengineyo.

Mashindano haya yanaonyesha uwezo mkubwa wa wanafunzi, na kazi kubwa inayofanywa na walimu ya ufundishaji.

Tambua kuwa Maahadi ya Qur’ani tukufu ni moja ya vituo muhimu vya Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya, inalenga kusambaza elimu ya Qur’ani na kujenga jamii yenye uwelewa na uwezo wa kufanya tafiti katika mambo tofauti yanayohusu Qur’ani tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: