Rais wa chuo kikuu Dhiqaar: Miradi ya Atabatu Abbasiyya tukufu inamafanikio makubwa na mfano mzuri wa kuigwa

Maoni katika picha
Kukamilika kwa ziara iliyofanywa na ugeni kutoka chuo kikuu cha Dhiqaar, ukiongozwa na rais wa chuo hicho Dokta Yahya Abduridhwa Abbasi, akiwa na wakuu wa vitivo na marais wa vitengo, ugeni huo umekuja kufuatia mawasiliano baina yao na idara ya mahusiano ya vyuo vikuu na shule chini ya kitengo cha mahusiano cha Atabatu Abbasiyya tukufu, wametembelea hospitali ya rufaa Alkafeel na majengo ya shule za Al-Ameed.

Ugeni umepokewa na mjumbe wa kamati kuu ya Atabatu Abbasiyya Dokta Abbasi Rashidi Mussawi, kituo cha kwanza wameenda katika hospitali ya rufaa Alkafeel, wakasikiliza maelezo kutoka kwa mkuu wa hospitali Dokta Jaasim Ibrahimi, ambae ameeleza huduma za kitabibu zinazotolewa na hospitali hiyo, pamoja na teknolojia ya kisasa na madaktari weledi walionao.

Mwisho wa ziara yake katika hospitali, rais wa chuo kikuu cha Dhiqaar ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Tumefurahishwa na tulicho shuhudia katika hospitali hii yenye teknolojia na vifaa vya kisasa, inatoa huduma bora kwa raia wa Iraq sawa na hospitali zingine za kimataifa duniani, tumekubaliana kuhusu kunufaika na maendeleo ya hospitali hii kupitia kuwaalika wanafunzi wa udaktari kutoka kwenye chuo chetu kuja kupata uzowefu katika hospitali hii, jambo hilo litasaidia sana katika masomo yao”.

Kisha ugeni ukaelekea katika majengo ya shule za Al-Ameed, ambako kuna shule ya awali, msingi na sekondari za wavulana na wasichana, pamoja na kwenye majengo yaliyozinduliwa mwaka huu wa masomo, ambako wamepokewa na rais wa kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya Dokta Ahmadi Kaabi, wakati wakitembea katika maeneo ya shule amewapa maelezo ya kutosha kuhusu huduma za malezi na elimu zinazo tolewa kwa wanafunzi wa shule hizo, pamoja na vifaa bora vya kufundishia walivyo navyo na ratima ya michezo na mapumziko.

Rais wa chuo amefurahishwa na alicho kiona kwenye majengo hayo ya malezi na elimu, amesema: “Tumeshuhudia majengo ya shule yaliyokamilika kila kitu, yamewekwa vifaa vya kila aina vya kufundishia, hakika mazingira ya shule ni mazuri, yanavutia na kutia moyo sekta ya elimu hapa Iraq, jambo hili linaonyesha namna Atabatu Abbasiyya tukufu inavyojali sekta hii, kuanzia ngazi ya shule za awali hadi chuo kikuu, nimatumaini yetu uzowefu huu uhamie kwenye mikoa mingine pia”.

Akaongeza kuwa: “Tumeona mazingira mazuri ya malezi, hakika haya ndio mazingira yanayotakiwa na wanafunzi wa Iraq, mazingira haya yanashinda mazingira yaliyopo kwenye vyuo vikuu vingine vya Iraq, wakati shule hizi ni za awali, msingi na sekondari, hali itakuaje kwenye ngazi ya chuo kikuu”.

Akamaliza maelezo yake kwa kusema: “Miradi ya Atabatu Abbasiyya tukufu inafanikio makubwa na mfano mzuri wa kuigwa, tunatarajia uzowefu huu uhamie kwenye mikoa mingine pia, tunaipongeza Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kazi kubwa na mafanikio mazuri”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: