Toleo ya arubaini na nne la jarida la Atwaau-Shabaad

Maoni katika picha
Kituo cha fikra na ubunifu chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimechapisha tolea la arubaini na nne la jarila la Atwaau-Shabaab, linaloandika mambo yanayohusu vijana, na kuangazia mambo muhimu ya kuwajenga.

Kiongozi wa kituo tajwa Ustadh Ridhwani Salami ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Toleo hili linamilango mbalimbali kutokana na mahitaji ya vijana, limeandikwa kwa njia mpya katika kuelezea changamoto zao, linajumla ya milango ishirini na sita, kuna mlando wa utamaduni, Dini, jamii, afya, michezo, maendeleo ya watu na mingineyo inayohusu vijana”.

Akafafanua kuwa: “Jarida hili ni sauti ya vijana, linawasilisha maoni yao na mitazamo yao, ni uwanja mzuri wa kushirikisha vijana na kuwaongoza katika maridhiano na maelewano, kuwatoa katika shaka na kuchanganikiwa na kuwaingiza katika imani na kujiamini, kuwatoa katika hali ya maneno na kuwaingiza katika vitendo”.

Tambua kuwa jarida hili, linasaidia kutangaza ubunifu wa vijana na kuwasaidia kifikra na kiujuzi, aidha linasaidia kutatua changamoto za kielimu na kikazi chini ya mafundisho ya Ahlulbait (a.s), na kutengeneza kijana mwenye mafanikio na ubunifu, na kukomaza uwelewa wa ukamilifu kiakili, kiroho na maadili.

Kumbuka kuwa jarida la Atwaau-Shabaab linapokea Makala mbalimbali na

kuziandika kwenye jarida, unaweza kuwasiliana nalo kupitia anuani za parua pepe zifuatazo: (ataa@alkafeel.net) au (info@alkafeel.net).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: