Shirika la Khairul-Juud limepata muitikio mkubwa katika maonyesho ya kibiashara ya Basra

Maoni katika picha
Shirika la Khairul-Juud la teknolojia ya kilimo cha kisasa Khairul-Juud chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, limepata muitikio mkubwa katika ushiriki wake wa awamu ya pili kwenye maonyesho ya kibiashara yanayofanyika Basra.

Msimamizi wa tawi na mkuu wa idara ya masoko katika shirika hilo Mhandisi Falaah Alfatla ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Huu ni ushiriki wetu wa pili katika maonyesho haya, tumekuja hapa baada ya kutoka kwenye maonyesho ya kilimo yaliyo fanyika Arbiil, yalikua na mafanikio na tulifikia malengo ya shirika, ushiriki huu ni muendelezo, aidha ni sehemu ambazo tunapata nafasi ya kueleza maendeleo ya Atabatu Abbasiyya tukufu, katika sekta ya viwanda na kilimo, na kukuza uwezo wa taifa katika upatikanaji wa chakula na uboreshaji wa maisha”.

Akaongeza kuwa: “Tawi limeonyesha aina tofauti za mbolea ambazo ni Rafiki kwa mazingira na hazina kemikali, ambayo imetimiza vigezo vya kimataifa, kuna mbolea kavu ya kuweka aridhini na mbolea ya mbaji ambayo hutumika kupuliza kwenye majani, kila aina ya mbolea inategemea aina ya mazao pia, pamoja na aina tofauti za chakula cha mifugo, aidha tumeonyesha vitakasa mikono na barakoa za aina mbalimbali, zinazo tumika mahospitalini na viwandani”.

Tawi limetembelewa na watu wengi waliokuja kuangalia bidhaa zetu, tumekua tukijibu maswali na kutoa ufafanuzi mbele ya viuongozi wa mashirika, serikali na raia wa Iraq kuhusu teknolojia tunayotumia katika kutengeneza bidhaa zetu ambazo zimekua zikichuana na bidhaa zinazozalishwa na viwanda vya kimataifa na zinaendana na maahitaji ya Iraq, zimekua na mafanikio makubwa kwa watumiaji.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: