Kifo cha mtoto wa Mtume (s.a.w.w) na roho yake iliyo baina ya mbavu zake

Maoni katika picha
Siku ya mwezi nane Rabiul-Awwal ni kumbukumbu ya kifo cha mbora wa wanawake wa duniani mtoto wa Mtume Muhammad (s.a.w.w) Fatuma (a.s) kwa mujibu wa riwaya ya kwanza, inayosema kuwa aliishi siku arubaini baada ya kifo cha baba yake.

Fatuma Zaharaa (a.s) baada ya kufa baba yake aliishi siku chache, akiwa ni mwenye huzuni na majonzi, kinacho onekana katika khutuba ya kiongozi wa waislamu (a.s) baada ya kumzika Mtume (s.a.w.w) kinaonyesha ukubwa wa mambo yaliyo mtokea, miongoni mwa maneno hayo ni: “Binti yako atakuambia undani wa umma wako, usimuuleze na tazama hali, wangapi wenye shida na hawajaona njia, Mwenyezi Mungu atahukumu naye ni mbora wa mahakimu”.

Katika siku kama ya leo mwaka 11 Hijiriyya zilisikika sauti za vilio katika nyumba ya Ali (a.s), wakazi wote wa Madina wakalia, wanaume kwa wanawake, watu wakafadhaika kama siku aliyokufa Mtume (s.a.w.w), wanawake wa bani Hashim wakakusanyika katika nyumba ya Fatuma (a.s) wakalia sana, watu wakamfuata Ali (a.s) akiwa amekaa na Hassan na Hussein wako pembeni yake wanalia, Ummu Kulhum naye akaja akiwa anasema: Ewe baba yangu, ewe mtoto wa Mtume wa Mwenyezi Mungu! Leo tumekukosa hatutakuona tena.

Watu wakakusanyika wakiwa wanalia, wanasubiri jeneza litolewe wamswalie, Abu Dhari akasema: Ondokeni hakika binti wa Mtume wa Mwenyezi Mungu ameahirishwa kutolewa hadi jioni.

Imamu Ali (a.s) alisimamia kumuosha na kumvisha sanda, akiwa na Asmaa wakati wa usiku, Kisha Ali akamswalia na akainua mikono juu na akasema: (Ewe Mola huyu ni mtoto wa Mtume wako Fatuma, umemtoa katika giza na kumtia kwenye nuru, ameangaza maili kwa maili).

Baada ya sauti kutulia na watu kulala, aliondoka kiongozi wa waumini na Abbasi, Fadhlu mtoto wa Abbasi na wanne, wakabeba muili huo mtakatifu, wakashindikizwa na Hassan, Hussein, Aqiil, Salmaan, Abu Dhari, Mikdad, Buraida na Ammaar.

Ali (a.s) akashuka ndani ya kaburi, akampokea binti wa Mtume (s.a.w.w) na kumlaza katika mwanandani, akasema: (Ewe ardhi nakukabidhi mtoto wa Mtume wa Mwenyezi Mungu, kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mwenye kurehemu, kwa jina la Mwenyezi Mungu na utukufu wa Mwenyezi Mungu na katika mila za Mtume wa Mwenyezi Mungu Muhammad bun Abdullah (s.a.w.w), kisha akasema: nimeridhia kama alivyo ridhia Mwenyezi Mungu mtukufu), halafu akatoka ndani ya kaburi, waliokuwepo wakaanza kulifukia, baada ya hapo Ali (a.s) akalisawazisha na ardhi, likawa halijulikani lilikua wapi na halitajulikana hadi siku ya kiyama.

Akawa kaondoka Zaharaa (a.s) akiwa na ham ya kukutana na Mola wake pamoja na baba yake, aliondoka akiwa na majeraha makubwa, ameenda kushtaki kwa Mola wake ili ahukumu baina yake na waliomdhulumu na kuchukua haki yake, amani iwe juu yake siku aliyozaliwa na siku aliyokufa na siku atakayo fufuliwa akiwa radhi mwenye kuridhiwa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: