Haram ya kipenzi wake imewekwa mapambo meusi katika kumbukumbu ya kifo chake

Maoni katika picha
Katika siku hizi kuna tukio linalo umiza nyoyo za waumini, nalo ni tukio la kifo cha Swidiqah Twahirah mbora wa wanawake wa duniani wa mwanzo na wamwisho Fatuma Zaharaa (a.s), kwa mujibu wa riwaya ya kwanza inayosema kuwa aliishi (a.s) siku arubaini baada ya kifo cha baba yake Mtume Muhammad (s.a.w.w).

Katika kuhuisha msiba huo mazingira ya huzuni yametanda katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), vitambaa vilivyo andikwa maneno yanayo ashiria huzuni vimewekwa sehemu mbalimbali katika eneo la haram tukufu.

Atabatu Abbasiyya imeandaa ratiba maalum ya kuomboleza yenye vipengele tofauti, kuanzia utoaji wa mihadhara ya kidini na uendeshaji wa majaalisi za uombolezaji sambamba na kujiandaa kupokea mawakibu za waombolezaji kutoka ndani na nje ya mji wa Karbala, zinazokuja kumpa pole bwana wa vijana Imamu Hussein na ndugu yale Abulfadhil Abbasi (a.s).

Kumbuka kuwa wapenzi na wafuasi wa Ahlulbait (a.s) dunia nzima wanaomboleza kumbukumbu ya msiba huu wa kifo cha mtoto wa Mtume Fatuma Zaharaa (a.s), fahamu kuwa kuna riwaya tofauti kuhusu tarehe ya kifo chake na sehemu lilipo kaburi lake (a.s), hii ni riwaya ya kwanza inayo sema kuwa alikufa (a.s) mwezi nane Rabiul-Thani, kwa mujibu wa riwaya hii anakua (a.s) aliishi siku arubaini baada ya kifo cha baba yake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: