Atabatu Abbasiyya tukufu inafanya majlisi za kuomboleza kifo cha Zaharaa (a.s)

Maoni katika picha
Ndani ya ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), imefanywa majlisi ya kuomboleza kifo cha mama wa Maimamu (a.s) na roho ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) bibi Fatuma Zaharaa (a.s), chini ya idara ya wahadhiri wa Husseiniyya katika Atabatu Abbasiyya tukufu, majilisi zitaendelea kwa muda wa siku nne.

Majlisi zimeanza siku ya Ijumaa mwezi sita Rabiul-Aakhar zitaendelea hadi mwezi tisa, chini ya mradi wa Ummul-Banina (a.s) unaohusika na matukio ya Maimamu wa Ahlulbait (a.s), likiwepo tukio hili, hufuatiwa na majlisi ya matam ambayo huongozwa na muimbaji Hashim Saidi, Muslim Haani, Muhammad Baagir Zaidi na Sajjaad Murdani.

Mzungumzaji ameongelea kwa undani tukio hili, pamoja na Maisha ya muhusika wa tukio, sambamba na kukumbusha yaliyomtokea bibi Fatuma Zaharaa (a.s) na nafasi yake katika Dini ya kiislamu, bila kusahau nafasi yake mbele ya Mwenyezi Mungu mtukufu na mbele ya Mtume Muhammad (s.a.w.w), na kauli za Mtume (s.a.w.w) na Maimamu watakasifu (a.s), pamoja na dhulma kubwa aliyofanyiwa na kuchukuliwa haki yake (a.s) na kuhimiza kushikamana na mwenendo wake (a.s) ambao ni mwenendo wa misingi ya uislamu na ubinaadamu.

Kumbuka kuwa wapenzi na wafuasi wa Ahlulbait (a.s) kila sehemu ya dunia wanaomboleza msiba wa mtoto wa Mtume Fatuma Zaharaa (a.s), kuna riwaya tofauti kuhusu tarehe ya kifo chake na sehemu lilipo kaburi lake (a.s), jambo hilo linaonyesha namna alivyo dhulumiwa na mitihani aliyopitia, hadi akamuhusia mume wake kiongozi wa waumini Ali (a.s), afiche kaburi lake na wala jeneza lake lisishuhudiwe na yeyote miongoni mwa waliomdhulumu na kuchukua haki yake, wakati wa kifo chake alikua na umri wa miaka kumi na nane kwa mujibu wa riwaya mashuhuri.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: