Chuo kikuu Alkafeel kinaomboleza kifo cha mtoto wa Mtume (a.s)

Maoni katika picha
Chuo kikuu Alkafeel chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kinaomboleza kifo cha mtoto wa Mtume na chemchem ya Uimamu bibi Fatuma Zaharaa (a.s) ndani ya ukumbi wa Shekh Tusi katika chuo hicho, na kuhudhuriwa na rais wake Dokta Nuris Dahani na wasaidizi wake pamoja na wakuu wa vitivo na marais wa vitengo, bila kusahau wanafunzi na watumishi.

Ratiba ya uombolezaji ilifunguliwa kwa Qur’ani tukufu, iliyofuatiwa na mhadhara kutoka kwa Shekh Jafari Dujaili, ameeleza misimamo na nafasi ya Zaharaa (a.s) wakati wa Mtume na wakati wa Uimamu, na namna alivyo tetea Uimamu na kuonyesha kua ni madaraka yatokayo kwa Mwenyezi Mungu na muendelezo wa kazi ya Utume.

Akaeleza pia baadhi ya fadhila za bibi Zaharaa (a.s) na historia yake takatifu, inayo faa kuigwa na mwanamke wa kiislamu, makamo rais wa chuo katika mambo ya utawala amesisitiza kuwa: “Majlisi hii ni sehemu ya ratiba ya chuo kikuu cha Alkafeel inayo lenga kuhuisha matukio ya Ahlulbait (a.s), na kuonyesha nafasi ya watakasifu (maasumina) katika kujenga jamii ya kiislamu”.

Hali kadhalika akaeleza baadhi ya sifa za pekee alizokua nazo bibi Zaharaa (a.s), sambamba na masomo na mazingatio yanayo patikana katika historia yake, ambayo sisi kama waislamu tunapaswa kuiga, na namna alivyofanikiwa kulinda jamii ya kiislamu isiharibike.

Kumbuka kuwa chuo kikuu Alkafeel huadhimisha matukio ya Maimamu wa Ahlulbait (a.s), sawa iwe tarehe za kuzaliwa au kufariki, kwa kufanya mambo tofauti kulingana na kila tukio.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: