Kitengo cha uhusiano katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kupitia idara ya mahusiano ya vyuo vikuu na shule, kimeandaa hafla ya kuzawadia watu walioshiriki katika kufanikisha mradi wa kuongoza waliopotea wakati wa ziara ya Arubaini, asubuhi ya Jumapili mwezi (8 Rabiul-Aakhar 1443h) sawa na tarehe (14 Novemba 2021m) ndani ya ukumbi wa Imamu Hassan (a.s) katika Atabatu Abbasiyya.
Hafla hiyo imehudhuriwa na mjumbe wa kamati kuu ya Atabatu Abbasiyya Ustadh Jawadi Hasanawi na baadhi ya marais wa vitengo na wasaidizi wao, pamoja na wawakilishi wa Atabatu Husseiniyya, Askariyya na wawakilishi wa jeshi kutoka wizara ya mambo ya ndani, vikosi vya ulinzi na afya vya hapa mkoani, na wawakilishi wa shirika la mawasiliano la Alkafeel, Asia sel na Iraq sel.
Hafla ilifunguliwa kwa Qur’ani tukufu iliyosomwa na Amiri Muhammad, kisha watu wakasimama na kusoma surat Fatha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq, halafu ukasikilizwa wimbo wa taifa na wimbo wa (Lahnul-Iba).
Ukafuata ujumbe kutoka kwa uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu uliowasilishwa na Ustadh Jawadi Hasanawi, akaanza kwa kushukuru na kutoa pongezi kwa kila aliyechangia katika mradi huu mkubwa wa kibinaadamu, akabainisha kuwa: “Utukufu wa kuwahudumia Maimamu wa Ahlulbait (a.s) na mazuwaru wao haulingani na kitu chochote, kuna hadithi nyingi kutoka kwa Maimamu zinazo himiza kutoa huduma hizi, Atabatu Abbasiyya tukufu imechukua jukumu la kuhakikisha inatoa huduma bora kwa mazuwaru, miongoni mwa ziara zinazopewa kipaombeza zaidi ni ziara ya Arubaini, hutumika kila mbinu katika kuhakikisha huduma zinatolewa kwa ubora mkubwa na ustadi wa hali ya juu, na miongoni mwa huduma ambazo hutolewa ni kuelekeza waliopotea, hii ni huduma ya kibinaadamu ambayo husaidia kumpa utulivu zaairu, tunatoa pongezi kubwa kwa kila aliyeshiriki kutoa huduma hiyo, tunatarajia itaendelea kuboreshwa zaidi katika miata ijayo”.
Baada ya hapo ukafuata ujumbe kutoka kwa viongozi wa jeshi (moja ya wadau wa mradi), ukawasilishwa na kapteni Ni’mah Muhammad, akasema: “Tunaishukuru Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kutupa nafasi ya kuhudumia mazuwaru, jambo ambalo tunalipa umuhimu mkubwa sambamba na kazi yetu ya kuhakikisha usalama wa mazuwaru, tumeshirikiana na watumishi wa kutoa huduma hiyo ya kibinaadamu inayosadia kumpa utulivu na amani zaairu wakati wa ziara ya Arubaini, kila tulicho fanya tunamuomba Mwenyezi Mungu akiandike katika kitabu cha vitendo vyetu, mambo yote tuliyo fanya hayawezi kulinganishwa hata kidoga na utukufu wa Imamu Hussein (a.s)”.
Baada ya ujumbe huo yakafuatia maonyesho ya kazi zilizo fanywa katika ziara ya Arubaini kwenye mradi huo, maonyesho hayo yaliongozwa na Ustadh Muntadhir Swafi kutoka idara ya uhusiano wa vyuo vikuu na mkuu wa kamati ya utendaji ya mradi huo, na Mhandisi Farasi Hamza Abbasi mkuu wa kamati ya ufundi ya idara ya mawasiliano katika Atabatu Husseiniyya tukufu, wameonyesha matukio (8992) ambapo jumla ya matukio (5976) yalihusisha (Watoto, watu wenye ulemavu, wagonjwa na wazee) ambao walikutanishwa na ndugu zao ndani ya muda mfupi.
Mwisho wa halfa hiyo ukawa ni kutoa zawadi kwa wahudumu wa mradi huo kutoka ndani na nje ya Atabatu Abbasiyya, miongoni mwa waliopewa zawadi ni kitengo cha habari cha Ataba tukufu kutokana na kazi kubwa kiliyofanya ya kuutambulisha mradi huo.