Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mji wa Najafu inaomboleza kifo cha bibi Zaharaa (a.s)

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mji wa Najafu chini ya Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya, imefanya majlisi ya usomaji wa Qur’ani awamu ya nne katika kukumbuka kifo cha Fatuma Zaharaa (a.s) kwa mujibu wa riwaya ya kwanza, katika kitongoji cha Huriyya mkoani hapo.

Majlisi imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu iliyosomwa na Akramu Saamir, halafu ukafuata mhadhara wa kielimu uliotolewa na Mheshimiwa Sayyid Muhammad Swadiq Khurasani, uliokua na anuani isemayo: (Fatuma Zaharaa “a.s” ni kiigizo chema), ameeleza sifa za bibi SwidiqatuL-Kubra (a.s), na mafundisho ya Mtume katika mwenendo wake.

Majlisi ikahitimishwa kwa maombolezo yaliyo ongozwa na Mhadhiri Shekhe Shibri Muallah.

Tambua kuwa majlisi kama hizi zinatokana na namna Maahadi ya Qur’ani chini ya Majmaa ya Qur’ani tukufu inavyo jali matukio hayo, hivyo hufanya harakati za usomaji wa Qur’ani katika wilaya na vitongoji tofauti na kuhimiza vijana waheshimu vizito viwili.

Kumbuka kuwa vikao vya usomaji wa Qur’ani vitaendelea kwa mujibu wa riwaya mbili zilizo baki (mwezi 13 Jamadal-Uula) na (mwezi 3 Jamadal-Aakhar) katika wilaya na vitongoji vya Najafu Ashrafu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: