Kuratibu mihadhara chini ya anuani (Kua muokozi)

Maoni katika picha
Wataalamu wa Alkafeel wa uokozi na ufundishaji wa matibabu chini ya kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, wanatoa mihadhara ya kielimu na kiutendaji chini ya anuani isemayo: (Kua muokozi) kwa wakufunzi wake, kwa lengo la kuongeza ujuzi katika sekta hiyo, na kuwafanya waendane na maendeleo ya sekta ya uokozi, pamoja na mbinu za kisasa.

Mtoa mada alikua ni Dokta Hussein Manati ameeleza falsafa ya ufundishaji wa michezo, amebainisha mambo mengi, miongoni mwa mambo hayo ni malengo na wajibu wa muokozi, njia za kulinda Maisha ya majeruhi katika ajali na majanga, kuandika tarehe na aina ya jeraha, na kukadiria huduma inayo endana na jeraha, jinsi ya kutumia watu waliopo katika eneo la ajali, jinsi ya kupunguza maumivu ya ajali, pamoja na kuzuwia ongezeko la majeruhi.

Aidha mhadhiri ameeleza nafasi ya muokozi, daktari na msaidizi, akafafanua njia za uokozi wa awali katika ajali, akafafanua vitendea kazi na umuhimu wake, akaeleza utokaji wa damu nyingi na ndogo, pamoja na jinsi ya kuamiliana na majeraha ya kuvunjika viungo na kusimama mapigo ya moyo.

Rais wa kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu Dokta Muhammad Hassan Jabiri amehudhuria kwenye muhadhara huo pamoja na Dokta Habibu Ali Twahiri Husseini mkuu wa kitivo cha malezi ya muili na elimu ya michezo katika chuo kikuu cha Karbala.

Kumbuka kuwa muhadhara huu ni moja ya mihadhara, semina na warsha zinazo fanywa na kitengo kwa watumishi wake, kwa lengo la kuboresha kiwango chao cha elimu na kuongeza uzowefu, jambo ambalo linasaidia kuboresha utendaji wao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: