Wito wa kushiriki katika awamu ya pili ya kongamano la Imamu Baaqir (a.s)

Maoni katika picha
Kamati ya maandalizi ya kongamano la Imamu Baaqir (a.s) awamu ya pili, imetoa wito kwa wasomi na watafiti waje kushiriki kwenye kongamano litakalo fanyika chini ya kauli mbiu isemayo: (Imamu Baaqir -a.s- ni mwezi ung’aao mjuzi wa kila kitu), litakalo fanywa mwezi mosi Rajabu sawa na tarehe mbili ya mwezi wa pili 2022m).

Mjumbe wa kamati hiyo Sayyid Aqiil Abdulhussein Yaasiriy ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kongamano linasimamiwa na kitengo cha habari na utamaduni na kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kama sehemu ya kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwake (a.s) na kuangazia turathi zake (a.s), kwani zimejaa misingi ya ubinaadamu na elimu”.

Akaongeza: “Mada za kongamano hilo zitajikita katika kuangalia upotoshaji wakati wa zama za Imamu Baaqir (a.s) na nafasi yake katika kupambana na upotoshaji huo, mada zifuatazo zitawasilishwa:

Kwanza: Kuharibika kwa maadili.

Pili: Kuharibika kwa uchumi.

Tatu: Kuharibika kwa fikra.

Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa namba zifuatazo:

+9647602323337
+9647602355555
au tuandikie barua pepe kwa anuani ifuatayo: conf@alameedcenter.iq
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: