Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la wanawake chini ya Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imefanya nadwa ya kumzungumzia Fatuma Zaharaa (a.s), kufuatia kumbukumbu ya kifo chake kwa mujibu wa riwaya ya kwanza.
Nadwa imefanywa ndani ya ukumbi wa wanawake ilikua na anuani isemayo: (Dhulma alizo fanyiwa bibi Zaharaa a.s), mtoa mada alikua ni Ustadhat wa Fiqhi katika Maahadi bibi Zainabu Najjaari, ameeleza yaliyojiri baada ya kifo cha baba yake Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w), akaeleza kuwa Ahlulbait (a.s) walieleza dhulma walizo fanyiwa, na Zaharaa anaumaalum katika dhulma alizo fanyiwa.
Akasisitiza umuhimu wa kutumia siku hizi kueleza dhulma alizo fanyiwa, na msimamo wake katika kufikisha ujumbe wa Dini ya kiislamu, kwa kusoma na kusikiliza mihadhara inayohusu turathi za Ahlulbait (a.s).
Kiongozi wa Maahadi bibi Mannaar Jaburi akasema kuwa: “Lengo la kufanya nadwa hii na zingine ni kumkumbuka mtakatifu huyu mbora wa wanawake wa duniani kwa kuangazia tabia zake, elimu yake na uchamungu wake, hakika tunahaja kubwa ya kusoma mwenendo wake mtakatifu na kufundisha vizazi vyetu ili waweze kufuata kiigizo chema”.