Kitengo cha malezi na elimu ya juu kinaendesha program ya (tunasoma ili tuwe hai) awamu ya tatu

Maoni katika picha
Kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kinaendesha program ya (tunasoma ili tuwe hai) awamu ya tatu.

Dokta Hassan Judhaili kiongozi wa kituo hicho amesema: “Tumeendelea na mfululizo wa vikao vya masomo katika awamu mpya tumeviita (barabara bora), imeanza program ya (tunasoma ili tuwe hai) awamu ya tatu kwa watumishi wa Ataba takatifu, akasema: (yanafundishwa masomo mengi) ni fursa ya watu wazima kujifundisha kusoma, kuandika na mambo mengine”.

Akaongeza kuwa: “Program inalenga kuboresha kiwango cha elimu kwa watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu, kwa kuwafundisha masomo tofauti yaliyo andaliwa na walimu mahiri kutoka kitengo cha malezi na elimu ya juu”.

Akasisitiza kuwa: “Program inahusisha mitihani ya kila siku katika mada zinazo fundishwa, pamoja na mitihani ya kuhitimu ambayo hutolewa mwishoni mwa program”.

Mkuu wa kitengo akasema kuwa “Program ya (tunasoma ili tuwe hai) ni sehemu ya mpango wa Atabatu Abbasiyya tukufu, unaolenga kuporesha kiwango cha elimu kwa watumishi wake, jambo ambalo linasaidia kuboresha huduma zao kila mmoja katika nafasi yake”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: