Kumbukumbu ya kifo cha mkarimu wa Ahlulbait bibi Fatuma Maasuma (a.s)

Maoni katika picha
Mwezi kumi Rabiul-Aakhar kwa mujibu wa moja ya riwaya, ni siku ya kukumbuka kifo cha bibi Fatuma Maasuma mtoto wa Imamu Mussa Alkadhim na dada wa Imamu Ridhwa (a.s), mwaka 201h katika mji wa Qum.

Alikosa amani (a.s) kuhusu hali ya kaka yake Imamu Ridhwa (a.s) toka alipoitwa na Ma-Amuun katika mji wa Khurasani, alikua na khofu baada ya kuambiwa na kaka yake Imamu Ridhwa (a.s) kuwa atakufa kishahidi katika safari hiyo ya kwenda Tusi.

Aliamua kusafiri (a.s) kumfuata kaka yake Ridhwa (a.s) akiwa anakusudia akutane nae akiwa hai, lakini shida ya safari na uchovu ulimdhofisha na kumkatisha safari, akaugua akiwa njiani, akauliza umbali uliopo kutoka sehemu alipo hadi katika mji wa Qum, wakati huo alikua amefika katika mji wa Sawa, akaambiwa: upo umbali wa Farsakh kumi sawa na -klm70-, akaamuru apelekwe katika mji wa Qum.

Riwaya zinaonyesha kuwa alibakia katika mji wa Qum siku 17, alikua anafanya ibada na kuswali katika sehemu inayo itwa (Baitu-Nuur) sasahivi ipo katika mji wa (Satiya).. akakata roho mwezi kumi Rabiu-Thani au (tarehe kumi na mbili ya mwezi huo kwa kauli nyingine) kabla hajakutana na kaka yake.

Alikufa (a.s) bila kumuona kaka yake, watu wa Qum wakahuzunika sana kwa kifo chake, wakaweka msiba na kuomboleza, wanawake wa kishia na wapenzi wake wakapata utukufu wa kumuosha bibi Maasuma na kumvisha sanda, ulipofika wakati wa kumzika viongozi wa sehemu hiyo wakaona bora azikwe sehemu maalum sio kwenye makaburi ya umma, walifanya hivyo kutokana na heshima kubwa waliyo mpa mtoto wa Imamu Alkadhim (a.s), hawakupenda azikwe pembeni ya makaburi mengine, jeneza lake lilishindikizwa na watu wengi sana katika mji wa Qum, waliojaa huzuni kwa kifo chake, wakambeba hadi kwenye makaburi ya (Babalaan) sehemu lilipo kaburi lake hadi sasa.

Kuna riwaya nyingi zinataja utukufu wa kumzuru bibi Fatuma (a.s), miongoni mwa riwaya hizo ni:

  • 1- Kutoka kwa Saad bun Saidi anasema: Nilimuuliza Abulhassan (a.s) kuhusu kaburi la Fatuma binti Mussa bun Jafari (a.s), akasema: (Atakaemzuru ataingia peponi).
  • 2- Imamu Jawaad (a.s) anasema: (Atakaezuru kaburi la shangazi yangu katika mji wa Qum ataingia peponi).
  • 3- Kutoka kwa Saad mtoto wa Imamu Ridhwa (a.s) anasema: (Ewe Saad, kwenu kuna kaburi letu) nikasema: (Kaburi la Fatuma mtoto wa Mussa?) akasema: (Ndio.. atakaemzuru akiwa anajua utukufu wake ataingia peponi).
  • 4- Imamu Swadiq (a.s) anasema: (Hakika Mwenyezi Mungu anaharam nayo ni Maka, na Mtume (s.a.w.w) anaharam nayo ni Madina, na kiongozi wa waumini (a.s) anaharam nayo ni Kufa, na sisi tunaharam nao ni mji wa Qum, atazikwa mtoto miongoni mwa watoto wetu aitwae Fatuma, atakae mzuru ataingia peponi).

Kutoka kwa Mussa Alkadhim (a.s) anasema: (Qum ni kiota cha Aali Muhammad na makazi ya wafuasi wao).

Imamu Ridhwa amesema kuhusu Maasuma (a.s): (Atakaemzuru akiwa anatambua utukufu wake ataingia peponi).

Haram ya bibi Fatuma Maasuma (a.s) ni moyo wa mji wa Qum na watu huenda hapo kwa wingi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: