Maukibu ya watu wa Karbala inaomboleza kifo cha Maasuma mbele ya malalo yake katika mji wa Qum

Maoni katika picha
Maukibu ya watu wa Karbala inaomboleza kifo cha Fatuma Maasuma (a.s) mbele ya malalo yake takatifu katika mji wa Qum, kwa kushirikiana na kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya.

Uombolezaji huu unahusisha maukibu ya matam na zainjiil, ni sehemu ya ratiba ya wageni waliokuja katika mji wa Qum, kuomboleza msiba huu uliotanguliwa na msiba wa bibi yake Zaharaa (a.s), ambaye alikufa tarehe kama hizi kwa mujibu wa riwaya ya kwanza.

Rais wa kitengo bwana Ni’mah Salmaan ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Maukibu ya watu wa Karbala huadhimisha matukio mbalimbali ndani na nje ya mji wa Karbala, ikiwa ni pamoja na kuomboleza msiba huu wa mkarimu wa Ahlulbait (a.s) ndani ya malalo yake takatifu, Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya zimeandaa usafiri wa kuwafikisha waombolezaji hadi kwenye mpaka wa Iraq na Iran, pamoja na kufanya mawasiliano na maandalizi ya vikao vya uombolezaji jambo lililofanywa na kitengo chetu”.

Akaongeza kuwa: “Wakati wa matembezi ya maukibu ya kuomboleza zimeimbwa kaswida za uombolezaji zilizo amsha hisia ya huzuni, wakati wa kuingia katika malalo yake takatifu kikafanywa kikoa cha kuomboleza, ambapo kaswida na tenzi tofauti zimesomwa”.

Tunatarajia kuwa na ratiba nyingine ya kuomboleza chini ya utaratibu wa maukibu, ndani ya haram hii takatifu na kwenye haram ya kaka yake Imamu Ali bun Mussa Ridhwa (a.s), ambapo atapewa pole kwa kufiwa na dada yake Maasuma (a.s).

Kumbuka kuwa maukibu hii ya kuomboleza ni utamaduni uliozoweleka kwa watu wa Karbala katika kuomboleza matukio ya Ahlulbait (a.s), nayo ni maukibu ambayo hupewa misaada na Ataba mbili Husseiniyya na Abbasiyya, katika harakati mbalimbali na matukio tofauti, likiwemo tukio hili.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: