Kuzawadia walimu walioshiriki katika mradi wa Qur’ani

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mji wa Najafu chini ya Majmaa ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, imefanya hafla ya kuzawadia walimu walioshiriki katika mradi wa Qur’ani wakati wa ziara ya Arubaini ya mwaka (1443h), zaidi ya mazuwaru (16000) kutoka mikoa tofauti walinufaika na mradi huo.

Mkuu wa Maahadi Sayyid Muhandi Almayali ameongea kuhusu jambo hilo, alianza kwa kukaribisha wahudhuriaji na kupongeza kazi iliyofanywa na kufanikisha mradi huo mtukufu wa Qur’ani, ambao ni miongoni mwa miradi inayopewa kipaombele sana na Maahadi. Mradi huu umekua na muitikio mkubwa mwaka baada ya mwaka, aidha Atabatu Abbasiyya inalipa umuhimu mkubwa tukio la kuwapongeza na kuwazawadia watu waliojitolea kufanya kazi kubwa ya kutumikia kitabu cha Mwenyezi Mungu.

Wazawadiwa wameshukuru sana na kupongeza idara ya Maahadi na Majmaa ya Qur’ani kwa kuwapa zawadi, jambo ambalo linawapa moyo wa kuendelea kutumikia Qur’ani tukufu.

Tambua kuwa mradi wa Qur’ani katika ziara ya Arubaini ulikua na aina zifuatazo:

  • Maonyesho ya Qur’ani ya mwaka wa pili.
  • Mradi wa kufundisha usomaji sahihi wa Qur’ani tukufu.
  • Mapumziko ya zaairu mdogo wa Qur’ani.

Kumbuka kuwa huu ni mradi muhimu katika Maahadi ya Qur’ani tukufu, kutokana na umuhimu wa Qur’ani katika makundi tofauti ya jamii na watu wa umri tofauti, sambamba na kuwa nafasi nzuri ya kujifunza mambo mbalimbali yanayo husu Qur’ani kwa mazuwaru wa Arubaini.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: