Chuo kikuu Al-Ameed kinafanya kongamano la pili la elimu ya utabibu

Maoni katika picha
Asubuhi ya Jumatano limeanza kongamano la chuo kikuu cha Al-Ameed awamu ya pili kuhusu elimu ya utabibu chini ya usimamizi wa chuo kikuu cha Al-Ameed kwa kushirikiana na chuo kikuu cha Alkafeel na hospitali ya Alkafeel na chuo kikuu cha Malezia (UKM).

Kongamano linaendeshwa katika chuo kikuu cha Al-Ameed, limefunguliwa kwa Qur’ani tukufu iliyosomwa na msomaji wa Ataba mbili Sayyid Hussein Halo, ukafuata ujumbe wa uongozi mkuu wa Ataba mbili tukufu uliowasilishwa na mjumbe wa kamati kuu ya Ataba tukufu na rais wa malezi na elimu ya juu Dokta Abbasi Rashidi Mussawi, amesisitiza kuwa Ataba tukufu inatoa kipaombele katika sekta ya malezi na elimu, kwa sababu ndio kitu muhimu kinacho jenga misingi ya ubinaadamu.

Kisha ukafuata ujumbe wa Waziri wa elimu ya juu, ulio wasilishwa kwa niaba yake na Dokta Swalahu Fatalawi rais wa chombo cha usimamiaji na upimaji wa elimu katika wizara, amepongeza watu wote waliochangia kufanikiwa kongamano hili, akawashukuru na kuwatakia mafanikio mema na akaomba kongamano litoke na maazimio yatakayo leta matokea mazuri katika safari ya elimu.

Chuo kikuu cha Al-Ameed kilikua na ujumbe uliowasilishwa na rais wa chuo hicho Dokta Muayyad Ghazali, amesema kuwa ufunguzi wa chuo kikuu cha Al-Ameed kama taasisi ya kielimu katika mkoa wa Karbala ni mafanikio makubwa kielimu kibinaadamu na kitabibu hapa nchini.

Baada ya hapo vikaanza vikao vya kuwasilisha mada za kitafiti, mwisho zawadi zikatolewa kwa watafiti walioshiriki kuwasilisha mada zao na utepe wa kufungua maonyesho maalum ya vitabu ukakatwa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: