Watumishi wa idara ya mitambo ya tahadhari na zimamoto chini ya kitengo cha majengo ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu inaumuhimu mkubwa wa kuweka mazingira salama dhidi ya moto, jambo hilo ni muhimu sana katika kuhakikisha usalama wa watu na majengo.
Kiongozi wa idara hiyo Mhandisi Muhammad Abdurasuul Hussein ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Mwanzoni mwa idara ilikua ndogo yenye kazi chache, lakini kutokana na kuongezeka ujenzi katika Atabatu Abbasiyya pamoja na mkakati wa kujitegemea, uliandaliwa mpango wa kuboresha kazi zote sambamba na upanuzi unaoshuhudiwa, tuliandaa jopo la wataalam wenye ujuzi na uzowefu mkubwa, lililosanifu na kufunga mitambo ya kutoa tahadhari na zimamoto”.
Akaongeza kuwa: “Jambo la amani na usalama ni msingi mkubwa wa kuepusha hasara ya watu na mali wakati linapotokea janga, sambamba na kulinda amani na usalama kwa ujumla, watumishi wa kitengo chetu wamepata mafanikio makubwa katika kuhakikisha usalama na kuzuwia majanga ya moto”.
Akafafanua kuwa: “Mitambo ya kuzuwia moto ni muhimu sana katika majengo, imewekwa kwa kushirikiana na kitengo cha usanifu wa majengo”.
Akamaliza kwa kusema: “Pamoja na kazi tulizo sema, watumishi wa idara yetu hupanga, hutengeneza na kufunga mitambo ya kutoa tahadhari na kuzuwia moto sambamba na kufundisha namna ya kuitumia”