Maukibu ya uombolezaji ya watu wa Karbala inafanya harakati ya kwanza ya uombolezaji katika mji wa Mash-Hadi

Maoni katika picha
Baada ya maukibu ya watu wa Karbala kuwasiri katika mji wa Mash-Had, imefanya majlisi ya kuomboleza katika Husseiniyya ya Karbalaiyya chini ya ratiba maalum iliyo andaliwa kwa na kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya katika Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya.

Muandishi wa Habari anayefuatana na maukibu hiyo amesema kuwa, uombolezaji ulikua ni kukumbuka kifo cha bibi Zaharaa (a.s) na mjukuu wake Fatuma Maasuma (a.s) miongoni mwa washiriki wa maombolezo hayo ni watu wa Karbala wanaoishi katika mji wa Mash-Had.

Akaongeza kuwa: “Baada ya usomaji wa Qur’ani ya ufunguzi alipanda mimbari msomaji wa tenzi za Husseiniyya Swaghiru Karbalai, akasoma kaswida na mashairi ya Karbalaiyya kwa mahadhi ya huzuni, zilizo amsha hisi za majonzi ya kuondokewa na mbora wa wanawake na sehemu ya moyo wa Mtume (s.a.w.w) na mumewe mgawaji wa pepo na moto na mama wa Maimamu (a.s) pamoja na dhulma na maudhi waliyo fanyiwa”.

Akafafanua kuwa: “Sehemu ya pili ya uombolezaji huo ilikua ni kuhuisha kifo cha Maasuma Ahlulbait (a.s), ambaye tupo katika siku za kuomboleza kifo chake”.

Tunatarajia kuendelea kufanya maombolezo ndani ya haram ya Imamu Ridhwa (a.s) ambapo kutakua na vipengele vingi, ikiwa ni pamoja na kumpa pole kwa kufiwa na dada yake Fatuma Maasuma (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: