Chuo kikuu cha Alkafeel chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimeshiriki katika siku ya kimataifa ya elimu ya juu, iliyo andaliwa na wizara ya elimu ya juu na tafiti za kielimu, nayo ni siku ya kutambulisha maendeleo ya kielimu na mafanikio yaliyopatikana katika vyuo vikuu hapa Iraq.
Rais wa chuo Dokta Nuris Dahani alikua na nafasi ya kuongea katika hafla hiyo, ameongea kuhusu mambo mbalimbali yanayo saidia kuboresha elimu hapa Iraq, aidha amezungumzia majengo ya chuo kikuu na mfumo wa mawasiliano sambamba na mchango wake katika mkakati wa malengo ya maendeleo endelevu, pamoja na kueleza majarida ya kielimu yaliyo chini ya chuo, mada nyingine ilihusu program ya Siraaj inayotumika kufundishia katika chuo, ameeleza pia mafanikio ya kiteknolojia yaliyopatikana.
Naye Dokta Aamir Abdul-Amiir muwakilishi wa wizara katika chuo kikuu Alkafeel amesema kuwa: Hakika hiki ni chuo cha pekee, kina mfumo bora wa kiteknolojia na majengo ya kisasa, kimekua kikichuana na vyuo vikuu vya Iraq bali kinavishinda, nakitakia mafanikio mema.