Kitengo cha malezi na elimu ya juu kimeanza kutumia program mpya ya (Albaswiratu-Naafidhah)

Maoni katika picha
Kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimeanza kutumia program ya (Albaswiratu-Naafidhah) katika shule za Al-Ameed, ngazi ya sekondari katika mwaka wa (2021/2022), na kuingizwa katika mfululizo wa program za malezi na elimu zinazo lenga kujenga misingi mizuri ya kibinaadamu kwa wanafunzi.

Kiongozi wa kitengo cha malezi na elimu ya juu Ustadh Wasim Abdulwahidi Naafi amesema: “Program hii ni sehemu ya juhudi za kitengo kuendana na maendeleo yaliyopo katika sekta ya malezi na elimu, nayo ni moja ya program mopya kwa wanafunzi wa shule za Al-Ameed”, akasema kuwa: “Program inahusisha wanafunzi wa ngazi ya msingi dara ya nne na la tano”.

Akaongeza kuwa: “Lengo kuu la program hii ni kubainisha mafundisho ya Ahlulbait hususan Abulfadhil (a.s), aliyesimama imara kumlinda Imamu Hussein (a.s) katika vita ya Karbala, pamoja na misingi mingine ya Dini ambayo ni sababu ya kuanzishwa kwa program hii, nayo ni muendelezo wa program za malezi katika shule za Al-Ameed”.

Msimamizi wa program Ustadh Swalahu Mahadi amesema: “Kitengo cha malezi na elimu ya juu kinajitahidi kufundisha misingi ya Dini na malezi kwa wanafunzi kuanzia shule za awali na msingi, kupitia program tofauti ikiwemo ya (Kanzul-Usbuui, Qiyamu-Tarbiyya, Tanmiyatu-Ruhiyya) na zinginezo”.

Akabainisha kuwa: “Ngazi ya sekondari inaprogram zifuatazo: (Alqiyamu-Tanmawiyya, barnaamiju- Almahadiy katika siku mia moja)” akasema: “Program ya (Albaswiratu-Naafidhah) ni ya ngazi ya sekondari, nayo ni muendelezo wa program zilizo tangulia, inalenga kutoa elimu bora kwa wanafunzi wa shule za Al-Ameed”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: