Maahadi ya Qur’ani tukufu inafanya semina kuhusu madhumuni ya Qur’ani katika Nahaju-Balagha

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’ani tukufu chini ya Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya inafanya semina ya Qur’ani kwa jina la (Madhumuni ya Qur’ani katika Nahaju-Balagha).

Shekh Jawadi Nasrawi mkuu wa Maahadi ya Qur’ani tukufu amesema: “Semina itakua na zaidi ya maustadhi (30) kutoka kwenye Maahadi na matawi yake watakao shiriki, tunatarajia watakua wanafundishwa kila siku ya Alkhamisi jioni ndani ya haram ya Atabatu Abbasiyya tukufu”.

Akabainisha kuwa: “Washiriki wa semina hii watapewa nakala ya kitabu cha Nahaju-Balagha, pamoja na kuwabainishia madhumuni ya Qur’ani yanayo bebwa na kitabu hicho, na kuonyesha uhusiano uliopo kati ya vizito viwili”.

Akasisitiza kuwa: “Maahadi imekua mstari wa mbele daima kufanya miradi tofauti na semina mbalimbali kwa ajili ya kutumikia vizito viwili, siku za mbele tutashuhudia semina zingine kwenye fani zingine”.

Kumbuka kuwa Maahadi ya Qur’ani tukufu chini ya Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya, kila baada ya muda hufanya jambo tofauti kuhusu Qur’ani, kwa lengo la kueneza utamaduni wa kusoma Qur’ani katika jamii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: