Mchoro, usanifu na ujenzi: watumishi wa kitengo cha majengo ya kihandisi wamejenga shule mbili ndani ya siku 70.

Maoni katika picha
Watendaji wa kitengo cha majengo ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya wamefanikiwa kuonyesha kuwa raia wa Iraq wanaweza kufanya kila kitu wanapotengenezewa mazingira mazuri, mafanikio ya hivi karibuni katika mkoa wa Baabil ni ushahidi tosha wa uwezo wa kitengo hicho, kimekamilisha ujenzi wa shule mbili ndani ya muda mfupi, kuanzia michoro, usanifu na ujenzi.

Rais wa kitengo Mhandisi Samiri Abbasi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Ujenzi wa shule hizi mbili ni sehemu ya mkakati wa kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, aidha ni sehemu ya kazi zenye mafanikio kuwahi kufanywa na kitengo chetu, siku (70) tu zimetosha kukamilisha ujenzi wa shule mbili kwa ubora mkubwa, unaokidhi vigezo vya wizara ya malezi na wenye mazingira mazuri ya masomo kwa wanafunzi”.

Akaongeza kuwa: “Ukubwa wa eneo la mradi ni mita (3650), ambapo zimejengwa shule mbili za msingi, moja ya wavulana na nyingine ya wasichana, kisha shule inavyumba vya madarasa, maabara, vyoo, vyumba vya ofisi (15) na sehemu ya bustani iliyopandwa miti ya aina tofauti, mradi umewekwa mifumo ya kisasa ya kutoa tahadhari na zimamoto pamoja na kamera”.

Mhandisi Samiri akabainisha kuwa: “Vifaa vyote vya lazima katika shule hizi mbili zimewekwa na mafundi wa mradi, ikiwa ni pamoja na milango, madirisha vifaa vya kufundishia na maosini”.

Kumbuka kuwa kitengo cha usimamizi wa majengo ya kihandisi, kinahusika na kujenga majengo ya Ataba tukufu, sambamba na kufanya ukarabati kwenye majengo tofauti yaliyochini ya Ataba takatifu, bila kusahau kazi za ujenzi zinazo endeshwa chini ya usimamizi wa Atabatu Abbasiyya.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: