Maukibu ya watu wa Karbala jioni ya siku ya Jumamosi mwezi (14 Rabiul-Aakhar 1443h) sawa na tarehe (20 Novemba 2021m) imehitimisha shughuli za uombolezaji na utoaji wa huduma zilizo anza zaidi ya siku saba zilizo pita katika malalo ya Imamu Ridhwa (a.s) hapa Mash-Had, ambapo ni kituo cha mwisho kabla ya kurudi Karbala, shughuli zote zimefanywa kwa kushirikiana na kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya.
Rais wa kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya bwana Riyadhi Ni’mah Salmaan ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Shughuli za mwisho zimefanywa ndani ya malalo ya Imamu Ridhwa (a.s), ambapo amepewa pole kwa kufiwa na bibi yake Zaharaa (a.s) na dada yake Maasuma Aali Muhammad bibi Fatuma Maasuma (a.s)”.
Akaongeza kuwa: “Harakati zimefanywa sambamba na matembezi ya kuomboleza kwa jila la watu wa Karbala, yalianzia katika barabara iliyo karibu na haram takatifu, waombolezaji walitembea wakiwa wamebeba bendera zinazo onyesha ishara ya huzuni kutokana na msiba huu, matembezi yakaishia katika haram takatifu ya Ridhwawiyya, huku wakiimba tenzi za kuomboleza”.
Akabainisha kuwa: “Kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya kimeshirikiana bega kwa bega na Atabatu Ridhwawiyya, katika kuainisha sehemu za kuanzia matembezi ya maukibu ya watu wa Karbala, pamoja na kuwabeba waombolezaji kutoka ma kwenda kwenye mpaka wa Iraq na Iran”.
Katika majlisi ya mwisho rais wa kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya amemshukuru kiongozi mkuu na watumishi wa Atabatu Ridhwawiyya kwa ushirikiano wao, pamoja na kuwakabidhi zawadi ya kutabaruku ambayo ni bendera ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
Kumbuka kuwa shughuli za kuomboleza hufanywa kupitia matembezi katika malalo ya bibi Maasuma (a.s) pamoja na kufanya majlisi katika husseiniyya ya nyumba ya Abbasi mjini Qum, na katika mji wa Mash-Had tumefanya majlisi mbili ndani ya Husseiniyya ya watu wa Karbala, na majlisi nyingine tulifanya katika malalo ya Sayyid Yahaya bun Zaid bun Ali bun Hussein (a.s), kuhusu utoaji wa huduma, tumegawa chakula katika mji wa Qum pamoja na kwenye malalo ya Sayyid Yahaya (a.s).