Ufunguzi wa awamu ya pili ya maonyesho ya turathi ya kimataifa

Maoni katika picha
Moja ya sehemu zilizopauliwa katika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu jioni ya Jumamosi (20 Novemba 2021m) sawa na tarehe (14 Rabiul-Aakhar 1443m), imeshuhudia ufunguzi wa awamu ya pili wa maonyesho ya turathi ya kimataifa, yaliyo ratibiwa na kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu chini ya anuani isemayo: (tabia tukufu).

Utepe wa ufunguzi umekatwa na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Mhandisi Muhammad Abdulhussein Ashiqar akiwa na makamo wake Mhandisi Abbasi Mussa na rais wa kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu Shekh Ammaari Hilali, pamoja na baadhi ya marais wa vitengo vya Ataba na waandishi, wadao na waandishi wa habari, na kundi la mazuwaru.

Kwa mujibu wa maelezo ya mjumbe wa kamati ya maandalizi Ustadh Khatwaat Muhammad Faalih aliyotoa kwa mtandao wa Alkafeel, amesema kuwa: “Maonyesho haya yanajumla ya mabango sabini yenye hati za Zukhuruf na Rasmi, yote yameandikwa kwa ubora mkubwa, baadhi ya maandishi yamepambwa kwa wino wa dhahabu halisi, kunazaidi ya waandishi ishirini wanaoshiriki kwenye maonyesho haya kutoka Iraq, Misri, Iran na china”.

Akaongeza kuwa: “Maonyesho haya yanafanywa kwa awamu ya pili chini ya idara ya Habari katika kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu, chini ya anuani isemayo (tabia tukufu), kama sehemu ya kuadhimisha Mtume Muhammad (s.a.w.w), maonyesho yatadumu kwa muda wa siku tano, tutaendelea kupokea mazuwaru watukufu asubuhi na jioni, chini ya usimamizi wa waandishi wa hati za kiarabu”.

Akamaliza kwa kusema: “Tunafanya kazi kwa msaada wa Atabatu Abbasiyya tukufu na uongozi wa kitengo kwa lengo la kutumikia turathi zetu za kiislamnu kwa njia mbalimbali ikiwemo hii ya maonyesho”.

Kumbuka kuwa awamu ya kwanza ya maonyesho haya ilipata muitikio mkubwa kutoka ndani na nje ya Iraq, yaliacha athari katika nafsi za mazuwaru jambo lililopelekea kuandaliwa maonyesho haya na kuongeza ushiriki wa vitu pamoja na shughuli za nje ya maonyesho.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: