Chuo kikuu Alkafeel kinazawadia wanafunzi wake waliofaulu katika kitivo cha famasia na kupongeza wahitimu wake

Maoni katika picha
Chuo kikuu Alkafeel chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimepongeza wahitimu wa mwaka wa masomo (2020 – 2021) na kutoa zawadi kwa waliofaulu, mbele ya makamo rais wa chuo Dokta Farasi Kaamil Muhammad na mkuu wa kitivo cha famasia pamoja na wazazi na walezi wa wanafunzi.

Makamo rais wa chuo ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kufanya hafla ya wanafunzi ni sehemu ya kupongeza kazi nzuri iliyofanywa na wakuu wa kitivo na walimu wao, katika kipindi cha masomo, wamefanya kazi kubwa, wanafaa kupongezwa kwa mafanikio haya na kuwaombea waendelee kutumikia taifa lao, tunatarajia walitendee haki jina wanalo tumia”.

Akaongeza kuwa: “Mafanikio haya yametokana na juhudi za wanafunzi na walimu, pamoja na msaada unaotolewa na uongozi wa chuo sambamba na ushirikiano mkubwa wa wazazi na walezi wa wanafunzi, ambao wamekua msaada mkubwa kwa vijana wao, na kustahiki kutambua mchango wao”.

Usfuur amebainisha kuwa: “Tunaheshimu wanafunzi wote, lakini tumegawa zawadi kwa wale waliopata nafasi za kwanza kutokana na upekee wao, chuo kitaendelea kuwasiliana na wahitimu wake wote na kutoa misaada kwao, tunawaombea mafanikio mema katika safari yao ya masomo”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: