Idara ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kushirikiana na shule za Al-Ameed za wasichana inaendesha program ya (Tukawazidishia uongofu) kwa ushiriki wa zaidi ya walimu (300).
Program inajumuisha mihadhara mbalimbali inayo lenga kujenga heshima ya mtu katika sekta ya malezi.
Hafla ya ufunguzi imeanza kwa mhadhara wa kifiqhi uliofuatiwa na filamu fupi inayo eleza umuhimu wa kufanya taklidi katika fiqhi, halafu likafuata jaribio lililokua na maswali (60) ya aina tofauti, fiqhi, aqida, hukumu za usomaji wa Qur’ani na historia.
Tambua kuwa program itaendelea kufanya vikao kila wiki.