Nadwa imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu, ukafuata ujumbe wa makamo rais wa chuo kikuu cha Basra Dokta Ali Hamdhwi Dhiyabi, amepongeza juhudi za Atabatu Abbasiyya tukufu katika kuchunguza jinai za kigaidi walizo fanyiwa raia wa Iraq na kuzitambulisha sambamba na kuonyesha athari zake katika nyanja tofauti, akasisitiza umuhimu wa kudumisha ushirikiano kati ya chuo kikuu cha Basra na Atabatu Abbasiyya tukufu katika uwanja wa elimu na utamaduni.
Ukafuata ujumbe wa mkuu wa kituo cha Iraq cha kuchunguza jinai za kigaidi Dokta Abbasi Quraishi, akaeleza nafasi ya kituo katika kuchunguza jinai za kigaidi, akaeleza umuhimu wa kuchunguza jinai hizo na akasema jambo hilo litasaidia kuzuwia vitendo vya kigaidi kama hivyo visijirudie tena hapa Iraq.
Halafu ikaanza rasmi nadwa chini ya usimamizi wa Dokta Ali Juudah Swabiihi, watoa mada walikua ni Dokta Bashiru Haadi, Dokta Thaairu Ghaalibu Naashi, Dokta Muhammad Najaah na Abdulhadi Ma’tuuq.
Miongoni mwa mada zilizo wasilishwa ni:
- - Jogrofia ya ugaidi (2003 – 2018).
- - Faida kuu za kuonyesha jinai za kigaidi.
- - Matokeo ya ugaidi katika miradi ya maendeleo.
- - Uchambuzi wa vitengo vya kigaidi.
Nadwa imeazimia kuongeza juhudi ya kuchunguza jinai za kigaidi, na kuongeza ushirikiano na taasisi za serikali kwa lengo la kuzuwia ugaidi, sambamba na kufanya utafiti wa namna ya kutambua viashiria vya ugaidi.
Ratiba ikahitimishwa kwa kuzindua kitabu cha (Jografia ya ugaidi nchini Iraq) kilicho andikwa na Atabatu Abbasiyya tukufu, kitengo cha kuchunguza jinai za kigaidi kwa kalamu ya Dokta Thaairu Ghaalib Naashi, kitabu hicho kimetaja vitendo vya kigaidi vya mwaka (2003 – 2018m).
Halafu vikatolewa vyeti vya ushiriki kwa washiriki wa nadwa na walio saidia kufanyika kwake.