Kumaliza kutengeleza sehemu zenye madini katika dirisha la bibi Zainabu (a.s)

Maoni katika picha
Mafundi wa kitengo cha kutengeneza madirisha ya makaburi na milango mitukufu katika Atabatu Abbasiyya, wamemaliza kutengeneza sehemu zenye madini za dirisha la bibi Zainabu (a.s) sehemu zinazo itwa (Dahanaat), nayo ni sehemu muhimu sana inayo fungua mlango wa kuingia katika hatua nyingine.

Rais wa kitengo na msimamiaji wa kazi hiyo Sayyid Naadhim Ghurabi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Mafundi wanaendelea na kazi ya kutengeneza dirisha kama ilivyo pangwa, walianza kutengeneza na kuunganisha sehemu za mbao katika umbo la mbao na kazi nyingine ni kutengeneza sehemu zenye madini, kwa ujumla kazi inaendelea vizuri kama ilivyo pangwa, tayali tumemaliza kutengeneza (Dahanaat) za dirisha”.

Akaongeza kuwa: “Jumla ya sehemu za madirisha (Dahanaat) kama zinavyo itwa na mafunzi ziko (14), zinazunguza dirisha tukufu pande zote, kila sehemu inamapambo ya umbo la mpira mdogo yapatayo (132) kila kiduara kina uzito wa (gram 122.5) ujazo wa duara moja ni (mlm 3), kuna aina za maduara (23), kuna aina ya (sm 143) na uzito wa (gram 87) na ujazo wa (mlm 6), kila kipande kinaurefu wa (198) na upana wa (sm 80), vipande hivo vya madirisha (Dahanaat) vinaumbo la upinde”.

Akabainisha kuwa: “Viduara na sehemu za kushika zimetengenezwa kwa silva na kuna ufito wa pambo uliotengenezwa kwa madini ya fedha halisi, upekee wa vipande hivyo ni mchanganyiko wa madini yaliyo tumika, yanayo lipa dirisha uwezo wa kuishi umri mrefu na kuhimili mabadiliko ya hali ya hewa”.

Akamaliza kwa kusema: “Kazi ya kutengeneza sehemu zenye madini zipo za aina tofauti kulingana na kila eneo, kila sehemu inayo kamilika inaonganishwa kwenye umbo la dirisha la mbao, tutaendelea kufanya hivyo hadi tumalize sehemu zote kwa idhini ya Mwenyezi Mungu mtukufu”.

Kumbuka kuwa sehemu zinazotiwa madini hua imara sana, sambamba na nakshi za mapambo zinazo wekwa kwenye kila eneo, nakshi na mapambo yanayo wekwa kwenye dirisha hili yanafanana na yale yaliyopo kwenye dirisha la Abulfadhil Abbasi na dada yake bibi Zainabu (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: