Makumbusho ya Alkafeel na Dhiqaar zimekubaliana kuweka mkakati wa pamoja na kubadilishana elimu na uzowefu

Maoni katika picha
Ugeni kutoka makumbusho ya Alkafeel na nakala-kale katika Atabatu Abbasiyya tukufu, umetembelea makumbusho ya Naswiriyya katika mkoa wa Dhiqaar, kwa ajili ya kuweka mkakati wa pamoja baina ya makumbusho mbili utakaosaidia kubadilishana uzowefu kati yao, na kujadili baadhi ya mambo yanayo husu makumbusho.

Ugeni umeongozwa na Ustadh Swadiq Laazim rais wa makumbusho ya Alkafeel, amesema kuwa: “Ugeni umehusisha baadhi ya watumishi wa kitengo, ziara hii ni sehemu ya safari za kielimu na tunatarajia kutembelea makumbusho tofauti za Iraq, ikiwemo makumbusho hii ambayo ni miongoni mwa makumbusho kubwa na yenye harakati na jina kubwa hapa nchini”.

Akaongeza kuwa: “Tumepokelewa na mkuu wa makumbusho Ustadh Sajjaad Abdulhassan, ametukaribisha kwa maneno mazuri na kututembeza katika korido za makumbusho, ametuonyesha mali-kale zilizopo katika makumbusho, aidha amejibu maswali ya wageni na kutoa ufafanuzi wa mambo mbalimbali yaliyo hitaji kufafanuliwa”.

Akabainisha kuwa: “Mwisho wa matembezi tumefanya kikao na mkuu wa makumbusho, tumeongea mambo tofauti yanayo husu sekta ya makumbusho, na umuhimu wa kuhamasisha jamii ya raia wa Iraq kuwa na utamaduni wa kutembelea makumbusho, kutokana na umuhimu wa jambo hilo wa kuongeza uelewa wa turathi za taifa kwa mwananchi, aidha tumeweka mkakati wa kubadilishana uzowefu katika sekta zote za makumbusho”.

Naye mkuu wa makumbusho ya Naswiriyya amesema: “Hii ni ziara ya kihistoria katika makumbusho yetu, tunaipa umuhimu mkubwa na tutajitahidi kufanyia kazi mambo tuliyokubaliana, ikiwa ni pamoja na kubadilishana uzowefu katika mambo ya makumbusho”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: