Atabatu Abbasiyya tukufu inaonyesha harakati muhimu za vitengo vyake

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu imetengeneza utaratibu wa kuonyesha harakati muhimu za vitengo vyake, kwa kuunganisha marais wa vitengo na kuwapa nafasi ya kueleza harakati zao ndani ya ukumbi wa Imamu Hassan (a.s) katika Atabatu Abbasiyya tukufu.

Shughuli hiyo imehudhuriwa na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Mhandisi Muhammad Ashiqar na makamo wake na wajumbe wa kamati kuu na marais wa vitengo, lengo ni kuonyesha kazi zinazo fanywa na vitengo hivyo, kwa kuangalia majukumu ya kila kitengo na utendaji wake, kwa kufuata ratiba maalum iliyo wekwa, kila siku tunaangalia shughuli za kitengo kimoja, tunatarajia kuangalia vitengo vyote hadi mwisho wa utaratibu huu.

Rais wa kitengo husika anaeleza shughuli zote zinazo fanywa na kitengo chake, pamoja na kazi zinazo fanywa na idara zilizo chini ya kitengo chake, mambo aliyofanikiwa kuyafanya na changamoto zilizopo katika utendaji wake, jambo hilo linasaidia kujenga uwelewa na kuangalia namna ya kutatua changamoto kwa pamoja na kufanya kazi kwa tim.

Baada ya kuonyesha shughuli zinazo fanywa hutolewa nafasi ya maswali na maoni kutoka kwa wahudhuriaji, kuanzia kwa katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu na marais wa vitengo vingine, rais wa kitengo husika anatoa majibu na kufafanua zaidi.

Kumbuka kuwa jambo hili linafanywa kutokana na maelekezo ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, kwa lengo la kuboresha utendaji wa kila kitengo na kuondoa changamoto, sambamba na kusikiliza maoni ya marasis wa vitengo na kuweka mikakati ya kuboresha huduma zaidi, kwa kuweka mkakati wa wazi na unaojulikana vizuri katika uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: