Upasuaji umemaliza tatizo la mgonjwa aliyekua anasumbuliwa na kuziba mirija ya uzazi

Maoni katika picha
Jopo la madaktari katika hospitali ya rufaa Alkafeel limefanikiwa kumaliza tatizo la mgonjwa mwenye umri wa miaka ishirini aliyekua anasumbuliwa na kuziba mirija ya uzazi, upasuaji huu sio wa kawaida kwa sababu umetumia teknolojia ya Nadhuur (bila kupasua sehemu ya muili) kwa weledi mkubwa.

Daktadi bingwa wa upasuaji wa njia ya mkojo na sehemu za uzazi Dokta Riyaadh Rashidi Aali Twa’amah amesema: “Zowezi limepata mafanikio makubwa”, akabainisha: “Tumetumia teknolojia ya Nadhuur, kazi yote imekamilika kwa muda wa saa mbili”.

Akabainisha kuwa: “Aina hii ya upasuaji ni ya kisasa zaidi na inahitaji umakini mkubwa”. Akasema: “Hospitali ya rufaa Alkafeel inavifaa-tiba vya kisasa na madaktari mahiri wanao iwezesha kutoa huduma hiyo”.

Akasisitiza kuwa: “Hali ya mgonjwa imeimarika baada ya kutolewa uvimbe uliokua unamsumbua katika mirija ya uzazi”.

Tambua kuwa Hospitali ya rufaa Alkafeel inatoa huduma bora daima kwa kutumia vifaa-tiba vya kisasa na madaktari mahiri kutoka ndani na nje ya nchi, jambo ambalo limeiwezesha kutoa ushindani mkubwa katika hospitali za kimataifa.

Kumbuka kuwa hospitali ya rufaa Alkafeel hualika madaktari bingwa wa magonjwa tofauti, sambamba na kupokea wagonjwa walio katika hali tofauti za maradhi yao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: