Hospitali ya Alkafeel imethibitisha mafanikio yake na kutaja sababu

Maoni katika picha
Jopo la madaktari wa upasuaji katika hospitali ya rufaa Alkafeel, limetaja mafanikio ya upasuaji kwa wagonjwa wake mbalimbali, na kusema kuwa teknolojia iliyopo na vifaa-tiba vya kisasa ndio sababu kubwa ya mafanikio hayo.

Daktari bingwa wa upasuaji Dokta Khalidi Siraji amesema: “Tunaendelea kufanikiwa katika upasuaji mbalimbali tunaofanya kwa wagonjwa tunao wapokea kutoka Karbala na mikoa mingine, ikiwa ni pamoja na upasuaji wa uti wa ngongo na ubongo”.

Akaongeza kuwa: “Uwezo wa hospitali na teknolojia yake ndio sababu kubwa ya kufanikiwa kwa upasuaji wetu, sambamba na weledi wa madaktari na wauguzi”. Akasisitiza kuwa: “Vifaa-tiba tunavyo tumia vinaupora mkubwa na vinakubalika kimataifa”.

Akasema: “Moja ya upasuaji wenye mafanikio tulimfanyia mzazi wa shahidi wa Hashdu-Sha’bi, tulirekebisha uti wa mgongo na kumuwekea ute wa kutengeneza, afya yake iliimarika baada ya tiba hiyo”.

Akaendelea kusema kuwa: “Kuna upasuaji mwingine alifanyiwa mama aliyekua na tatizo la ute kwenye viungo vyake tofauti na kwenye uti wa mgongo, akafanyiwa upasuaji na kuwekewa ute wa kutengenezwa ambapo afya yake iliimarika baada ya matibabu hayo”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: