Tambua majarida ya kitengo cha maarifa kiislamu na kibinaadamu

Maoni katika picha
Kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kinamiliki majarida ya turathi, ambayo huandika mambo yanayohusu turathi za kiislamu, yamepewa kibali na wizara ya elimu ya juu na tafiti za kielimu hapa Iraq.

Majarida hayo hutolewa na vituo vilivyo chini ya kitengo hiki kwa miaka mingi, kuna jumla ya majarida matatu, nayo ni: (Turathi za Karbala) linatolewa na kituo cha turathi za Karbala, (Turathi za Hilla) linatolewa na kituo cha turathi za Hilla, (Turathi za Basra) linatolewa na kituo cha turathi za Basra.

Kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu kinatarajia kutoa majarida mengine mawili hivi karibuni, moja litatolewa na kituo cha Najafu kwa jina la (Jarida la turathi za Najafu), na lingine litatolewa na kituo cha turathi za kusini, kwa jina la (Jarida la turathi za kusini).

Pamoja na tuliyosema kuna majarida mengine ya kawaida yanayotolewa na kitengo hiki, kama vile jarida la (Alkhatwah), jarida la (Radu-Shamsi) na jarida la (Ghadhwiriyyah), tutayaelezea yote katika ripoti ijayo.

Kumbuka kuwa machapisho ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya ni kitovu cha utafiti kwa watafiti wa mambo ya turathi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: