Kuanza kwa moja ya hatua za ukarabati wa mlango wa Imamu Kadhim (a.s)

Maoni katika picha
Watumishi wa mradi wa kukarabati milango ya Atabatu Abbasiyya tukufu katika haram ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), wameanza moja ya hatua muhimu za ukarabati wa mlango wa Imamu Mussa Alkadhim (a.s), uliopo upande wa kusini magharibi ya haram tukufu, nao ni moja ya milaango maalum ya wanawake, sehemu hiyo pia inamlango wa kuingia katika mgahawa (mudhifu) wa Ataba takatifu.

Awamu hii imeanza kwa kuweka nguzo za chuma katika vizingiti vya mlango kama sehemu ya kujiandaa kuweka nakshi na mapambo, baada ya kumaliza kuutengeneza upya kwa namna ambayo inaendana na turathi za zamani na za sasa, pamoja na kulandana na milango mingine na nakshi zilizopo katika haram.

Hatua hii imeanza baada ya kumaliza hatua nyingi, ikiwemo kuweka marumaru sakafu na ukuta pamoja na kuupamba kwa kashi Karbalai sambamba na kuweka mifumo yote inayo hitajika kama vile umeme, vipaza sauti, kamera na mingineyo.

Tambua kuwa mlango wa Imamu Kadhim (a.s) unatofautiana na milango mingine yote ya Atabatu Abbasiyya tukufu, hauelekea kwenye uwanja wa haram moja kwa moja, jambo ambalo linahitaji usanifu unao endana na umbo lake, na kufanana na milango mingine ya Ataba tukufu, inayo elekea kwenye uwanja wa haram tukufu, ikiwa katika mfumo wa kisasa.

Kumbuka kuwa kazi hii ni sehemu ya mradi wa kukarabati milango inayo elekea katika uwanja wa haram tukufu (iliyokua zamani ndio milango mikuu), pamoja na mlango mkuu unao elekea kwenye uwanja wa haram kwa kutoka nje, kuanzia mlangoni hadi kwenye mlango wa zamani unaopakana na uwanja wa hara tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: